visa

Shiboub Awavuruga UD Songo

Wachezaji wa Simba akiwemo Shiboub Sharaf (kushoto), Kagere (katikati) na Chama (kulia).

MCHEZO wa Ngao ya Jamii kati ya Simba na Azam umewatibulia Ud Songo baada ya kocha wao kubadilisha aina ya mazoezi na utaratibu.

 

Kocha wa Songo ambayo ni moja ya timu mahiri nchini Msumbiji kwa sasa Nacir Armando, aliwatuma watu wake kwenye mchezo wa Simba dhidi ya Azam, lakini kiwango ambacho kilionyeshwa na wachezaji wa Simba kimemshtua na kumzidishia presha.

 

Simba walivaana na Songo wiki mbili zilizopita kwenye mchezo wa hatua ya awali wa Klabu Bingwa Afrika na kumaliza kwa suluhu na sasa timu hizo zinarudiana Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

Simba imekuwa timu tishio kwa siku za hivi karibuni baada ya kufanikiwa kufika hatua ya robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika msimu uliopita na kuipa Tanzania neema ya kuongezewa timu kwenye mashindano hayo.

Mitandao ya Msumbiji, iliripoti jana kwamba awali kocha wa timu hiyo aliamini kuwa mchezo utakuwa kama ule wa awali kule kwao lakini baada ya kuona kiwango cha Simba ilipovaana na Azam na kuona wingi wa mashabiki amebadilisha gia.

 

Lakini jana Msemaji wa Simba, Haji Manara alisisitiza jana kwamba wamejiandaa kuonyesha kiwango kikubwa chenye hadhi ya mabingwa kwenye mechi hiyo.

 

Taarifa hizo zinasema kuwa alikuwa ameomba mchezo wake dhidi ya Nampula unaopigwa leo usogezwe mbele ili wapate muda mwingi wa maandalizi, lakini ameamua wacheze ili aweze kuona kile ambacho wachezaji wake wamekielewa kuanzia walipobadilisha utaratibu.

 

“Timu imekuwa ikifanya mazoezi usiku na mchana hii ni hofu kuwa hawajui Simba watapanga mechi saa ngapi, lakini pia kocha amebadilisha mambo mengi baada ya kuona mechi ya Simba na Azam.

“Ameona ubora wa wachezaji wa Simba akiwemo Shiboub Sharaf, lakini pia safu ya ulinzi ilicheza vizuri sana kuliko ilivyocheza huku hivyo tumejiandaa vyema,” kilisema chanzo hicho.

 

Hata hivyo, Meneja wa Simba Patrick Rywemamu, alipozungumza na Championi jana alisema kwa ufupi kuwa: “Sisi tulicheza soka kulingana na program ya mwalimu, tunaamini kuwa tunaweza kufanya vizuri sana kwenye mchezo huo,” Patrick.

 

Simba wamepania kuwachakaza Songo na kumaliza mchezo huo kwa kishindo wakilinda rekodi yao ya uwanja wa nyumbani kwenye mashindano hayo yenye fedha zaidi kwa ngazi ya klabu Afrika.

Haji Manara AWEKA WAZI KUACHIA NGAZI Simba “Sitokaa Milele”/ Nawatakia Kheri YANGA
Toa comment