×

Mashine Nyingine Zinakuja Yanga Baada ya Usajili wa Mudathir Yahya

Mudathir Yahya.

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa baada ya kufanikisha usajili wa Mudathir Yahya na kutambulishwa rasmi, bado kuna mashine nyingine watazitambulisha hivi karibuni mara baada ya kukamilisha usajili wao.

Yanga jana Jumamne walimtambulisha aliyekuwa kiungo wa Azam FC, Mudathir Yahya ambaye tayari ameshajiunga na timu ya Yanga ambayo inashiriki michuano ya Mapinduzi inayoendelea kutimua vumbi visiwani Zanzibar.

Akizungumza na Spoti Xtra, Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe alisema kuwa mara baada ya kumtambulisha mchezaji huyo bado watafanya usajili wa wachezaji wengine na kuwatambulisha kwani bado hawajamaliza usajili wao katika dirisha hili huku akitamba kuwa utakuwa usajili wa maana.

“Ni kweli tayari tumeshamtambulisha Mudathir lakini bado hatujamaliza kwenye suala la usajili kwani tutafanya usajili mwingine wa maana kupitia dirisha hili dogo na tutawatambulisha hivi karibuni vifaa vyetu.

“Usajili tutakaoufanya utakuwa ni funga kazi hivyo watu wanatakiwa kuwa watulivu kwani hatujamaliza na tutawafurahisha kama kawaida yetu,” alisema kiongozi huyo.

STORI NA MARCO MZUMBE, CHAMPIONI JUMATANO

#EXCLUSIVE: SOPHIA AMELOWA AMUOMBA MSAMAHA HARMONIZE | HOTPOT

Leave a Comment