Shigongo Amshauri Trump kusitisha uamuzi wake wa kuzuia misaada Afrika – Video
Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo amemshauri Rais wa Marekani, Donald Trump kusitisha uamuzi wake wa kuzuia misaada kwa nchi za Afrika, kwa sababu akifanya hivyo Waafrika wengi watapoteza maisha.
Akiwa nchini Marekani kikazi, Shigongo amesema misaada ya Marekani kwa nchi za Kiafrika, inasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na changamoto mbalimbali zikiwemo za kiafya kwa nchi za Kiafrika ikiwemo Tanzania.
Akitolea mfano wa PEPFAR, Shigongo amesema msaada huo ulikuwa unazisaidia nchi za Kiafrika kuwatibu waathirika wa HIV/AIDS kwa kuwezesha kupatikana kwa dawa za kupunguza makali ya Virusi vya Ukimwi kwa Waafrika wengi na kwamba kusitishwa kwa misaada hiyo, kutasababisha vifo vya Waafrika wengi ikiwemo Watanzania.