The House of Favourite Newspapers

Shoga: Ukimkomoa akachepuka utafanyaje?

0

Na Sophia Ma’mdogo (0713-133 633), Uwazi, Mapenzi na Maisha

HALO halo shoga weee naona kiroho kinawadunda baada ya kuufunua ukurasa huu na kujiuliza leo kombora linaangukia kwa nani? Narudia, sipo kwa ajili ya kuwarusha roho bali mtajirusha wenyewe kutokana na tabia zenu mbaya wanaizaya vizabizabina, mpo? Vijana wa leo wanasema shobo dundo, sipendi niwe muongeaji sana ila ujumbe ukufi kie shoga yangu au siyo? Shoga kuna kitu kimenikaa hapa, kimenifi ka hapa! Nikisema hapa namaanisha kooni, kula siwezi, kukaa kimya siwezi najikuta mdomo ukijiachia wenyewe, heee heeeiiyyaaa! Baada ya hayo shoga tuingie kwenye mada yetu ya leo.

Shoga yangu leo nazungumza na wewe mwanamke mwenzangu usiye na haya usiyejua wakati gani wa kumkomoa mumeo, jamani wanawake wengine sijui tumerogwa na mchawi aliyeturoga kaugua wendawazimu, sijui nani wa kutuponya! Loo! Kuna kitu kimoja jana kilinikera na kunifanya niwarudishe kwenye unyago ule tuliofundishwa, juzi nikiwa nakwenda zangu mjini nilipanda kwenye daladala na kukaa siti ya nyuma, mbele yangu kulikuwa na wanawake wawili waliokuwa wakiongea mambo ya ndani bila aibu, shoga hivi wapo watu wa aina hii kumbe!

Basi kutokana na maongezi yao ndiyo maana nikajiuliza kama waliochezwa wakachezeka ina maana wamesahau mafunzo ya unyagoni, itakuwa wewe unayewekwa saa mbili mbele ya watu eti kitchen party! Hivi kwanza wewe mwanamke, eeh jamani aibu umeiweka wapi kufi kia hatua ya kuyasema maneno ya ndani mwako, maneno yako na mumeo ukayaingiza ndani ya daladala bila hata kugongwa na mshipa wa aibu, umerogwa?

Nilimsikia akisema eti alikorofi shana na mumewe na kumsubiri kitandani ndipo alipomkomoa kwa kumkaripia, alipomgusa alimjia juu na
kumwambia amkome! Weweee mwanamke ndivyo mlivyofundishwa unyagoni kumfanyia mumeo katika uwanja wa sita kwa sita pale mnapokosana. Unajua madhara ya kumnyima kucheza mechi? Kibaya zaidi upumbavu ulioufanya unamweleza rafi ki yako bila aibu, pengine hata hajui ndoa ni nini, majibu yake mepesimepesi tu eti; “Shoga tena mkomeshe, wanaume wa siku hizi wamezidi.”

Kweli hizi ndizo moja ya sababu za kumfanya mumeo atembee na dada wa kazi? Wewe umekataa pengine wiki ukijua unamkomoa, mwanaume hakomolewi shoga, ukimkomoa wenzako wanafanya kweli ati! Kuna wenzako wametega tu pembeni ukijifanyaunamkomoa wao wanampa tena bureee hakuna cha kukomoana, upo? Kama huamini hebu jaribu kumkomoa wiki tu kama hujaishia kutoa machozi hadi yajae bahari, heee heee heeeiya!!! Shoga nataka tuzungumze kitu kimoja kwako na ujue uliweke kichwani mwako, upo?

Shoga ni kosa kufungua mahakama mkiwa uwanjani tena kiwanja cha sita kwa sita kama siyo tano kwa sita, mwenzio anataka wewe ndiyo unaanza;
“ohhh unajua,” ajue nini mpe chakula chake cha usiku mashtaka baadaye. Shoga, unamnyima mumeo haja zake akamalize wapi kwa mfano? Akipata nyumba ndogo inayomjali uanze kupiga kelele. Hebu wanawake tuache akili za punda wa dobi, mumeo akikukosea pataneni lakini siyo kumpa adhabu ya kumnyima chakula cha usiku. Kwa leo ni hayo tu, tukutane tena wiki ijayo kwa mada tamu zaidi. Kama una maoni usisite kunitumia meseji tu kwa namba hiyo hapo juu nitaipata!

Leave A Reply