Shoo ya ‘Piga Nikupige’ Dar Live Yaacha Gumzo – Video
USIKU wa mpambano wa bendi tatu za taarabu na wasanii wa singeli uliokwenda kwa jina la Piga Nikupige uliofanyika jana (Jumatano) siku ya Idd Al Haj ulikuwa ni zaidi ya burudani kwa jinsi makundi hayo yalivyofunikana katika kuwanogesha mashabiki waliofurika ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, Dar.
Bendi zilizotifuana katika mpambano huo zilikuwa ni Hurricane, Jahazi na Zanzibar Stars Modern Taarabu ‘Wana Nakshinakshi’ ambapo baada ya mtifuano huo wasanii wa singeli nao walipewa nafasi ya kuonyesha umahiri wao.
Burudani hizo ziliwafanya mashabiki waserebuke mwanzo-mwisho kufuatia kunogeshwa na burudani hiyo.
Mwimbaji wa singeli, Pazo Mreno, akichagiza mashabiki.
PICHA: RICHARD BUKOS / GPL
Comments are closed.