The House of Favourite Newspapers

Simba Watambulisha ‘Jembe jipya’ Onana kutoka Cameroon

0

Rasmi uongozi wa Simba Sports Club, umemtambulisha mchezaji wao mpya Willy Essomba Onana(23) , ambaye amesajiliwa ili kuongeza nguvu katika kikosi cha wekundu wa msimbazi simba kuelekea msimu ujao wa soka.

 

Simba wamefanikiwa kumsajili kiungo huyo mshambuliaji) raia wa Cameroon kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya Rayon Sports ya nchini Rwanda.

 

Onana ambaye amefanikiwa kuwa na msimu mzuri kwenye Ligi kuu Rwanda alimaliza msimu wa 2022/23 kama mfungaji bora akiwa na jumla ya magoli 16 anatinga ndani ya viunga vya wekundu wa msibazi, Simba kuchukua nafasi ya Mghana, Augustine Okrah ambaye ameondoka.

Leave A Reply