Simba Yaitungua Mtibwa, Yanusa Ubingwa!

BAADA ya kupata matokeo mabaya kwa michezo miwili mfurulizo, Timu ya Simba imeibuka na ushindi mnono wa bao 3 -0 dhidi ya Wakata Miwa wa Turiani, Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara ambao umpigwa katika Uwanja wa Uhuru jijini dar es salaam leo, Alhamisi, Mei 16, 2019.

Mabao ya Simba yamefungwa na  John Raphael Bocco (dakika ya 33), Mwamba wa Lusaka Clatous Chama (dakika ya 48) na Emmanuel Okwi (dakika ya 56) yametosha kuirejea Simba kileleni mwa msimamo wa ligi wakihitaji pointi 5 katika mechi zilizobaki ili kuutangaza ubingwa wa pili mfululizo wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Stand United ‘Chama la Wana’ wamechukua pointi tatu kwenye Dimba la Kaitaba mjini Bukoba baada ya kuitungua Kagera Sugar bao 1-3.

Matokeo ya mechi mbili za leo yameirejesha Simba kileleni huku Stand United ikizidi kunogesha vita ya kukwepa kushuka daraja, ikipanda kutoka nafasi ya 17 hadi nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi.

Loading...

Toa comment