Simba Yashtukia dili la Mtibwa na Yanga

Kikosi cha timu ya Mtibwa.

SIMBA inajua kwamba Mtibwa itakomaa leo Alhamisi ndani ya Uwanja wa Uhuru lakini Kocha Patrick Aussems amesisitiza ni ya kufa kupona lazima mtu apigwe kwa namna yoyote ile.

Simba wanahaha kusaka pointi nane ambazo zitawafanya wafikishe pointi 90 na kujihakikishia nafasi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

 

Kwa sasa wana pointi 82 wakiwa nafasi ya pili kwenye msimamo nyuma ya Yanga wenye 83. Aussems amesisitiza kwamba anajua wakipoteza mchezo huo watatoa faida kwa Yanga ambayo Kocha wao, Mwinyi Zahera amedai wanaweza kufanya sapraizi msimu huu tena dakika za mwisho.

 

Katika kusaka pointi nane hizo Simba wana michezo miwili na Mtibwa yenye pointi sita, watacheza leo Dar katika Uwanja wa Uhuru na Morogoro, Singida United miwili pamoja na mmoja dhidi ya Ndanda FC.

 

Aussems ameliambia Spoti Xtra, kwamba; “Tulitarajia kwenye mechi na Kagera na Azam tupate matokeo mazuri lakini ikashindikana, tangu hapo nguvu tumeelekeza kwenye mechi hii na Mtibwa kisha na Ndanda (Jumapili) tukishinda hizi ninaamini tutakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kutimiza kile tulichokipanga.”

Kikosi cha timu ya Simba SC

“Kwa sasa ni mechi ngumu sana zilizo mbele yetu kwa sababu tunaenda mwisho wa ligi, lakini lengo ni kushinda mechi hizo na tupate pointi nane kwa ajili ya kujitangazia ubingwa,” alisema Aussems.

 

Straika mwenye uchu wa mabao Meddie Kagere amesema; “Mtapata majibu ndani ya uwanja kwani mimi huwa sipendi sana kuongea napenda kuonyesha vitendo na vitendo ni bora kuliko maneno.”

 

Kocha wa Mtibwa Sugar, Zubeir Katwila amesema: “Mechi itakuwa ngumu kwa kila upande, lakini nimewapa mbinu wachezaji wangu kuhakikisha kwamba wanawatibulia Simba katika mechi hii na kuchukua pointi zote tatu.”

 

Msimu uliopita Simba ilishinda mchezo mmoja uwanja wa Jamhuri na ule uliopigwa Taifa waligawana pointi moja.

Loading...

Toa comment