
KLABU ya Barcelona imemuweka kando beki wake mkongwe, Dani Alves katika michuano ya Europa League, huku Pierre-Emerick Aubameyang na Adama Traore wakipenya kwenye kikosi hicho.
Barcelona inatarajiwa kucheza michuano ya Europa League mwezi huu baada ya kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya 2021- 22.
Klabu hiyo imewasilisha majina ya wachezaji watakaoshiriki michuano hiyo kwenye Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA), huku Alves akitajwa kutokuwa kwenye kikosi hicho.
Majina mapya ambayo yameongezwa ni pamoja na Aubameyang, Traore na Ferran Torres ambao wametua kikosini hapo kipindi cha usajili wa dirisha dogo Januari mwaka huu, pamoja na wachezaji wengine kutoka Barcelona B akiwemo IliasAkhomach, Astralaga Balde, Arnau Comas, Jandro, Gavi, Alvaro Sanz na Arnau Tenas.
Imeelezwa kuwa Alves ameachwa kwa sababu nyingi hasa uwepo wa mabeki kama Sergino Dest, Oscar Mingueza, Ronald Araujo na Sergi Roberto.
Huku sababu nyingine ikitajwa kuwa atatumika zaidi kwenye La Liga kuhakikisha Barcelona inafanikiwa
kutimiza malengo
ikiwemo kubeba
ubingwa.