SIMBA: POLOKWANE CITY WAMEKIUKA TARATIBU KUMSAJILI BOCCO

Mshambuliaji wa Simba, John Bocco ameiingiza  vita klabu yake ya Simba na ile Polokwane City inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini baada ya kusaini mikataba na klabu hizo.

 

Baada ya Simba jana kuachia picha zikimuonyesha Bocco akisaini mkataba mpya ndio habari za nahodha huyo kusaini mkataba na Polokwane zikaibuka.

 

Uongozi wa Simba kupitia kwa Mtendaji mkuu wa Simba, Crescentius Magori umesema ni kweli Bocco alisaini mkataba wa awali, lakini hakufuata taratibu.

Magori alisema anajua kabisa kwamba mchezaji huyo alisaini mkataba wa awali, lakini hilo halikuwazuia wao kumpa mkataba mpya kwasababu bado alikuwa katika mkataba wao.

“Polokwane walikosea kwa sababu hawakufuata taratibu, walijua tayari tumeshamsaini, lakini wao nao walikuwa wanataka kama ushindani na sisi, hata huyo wakala sisi tulimuambia kabisa kwamba tayari tumemalizana,” alisema Magori.

Aliongeza kwamba kuhusu suala la mkataba wa awali hata wao walimsainisha mshambuliaji wa Ndanda, Vitalis Mayanga, lakini siyo mchezaji wao.

 

#E FM Radio

Toa comment