The House of Favourite Newspapers

SITASAHAU NILIPOLALA NA MWANAMKE JUU YA KABURI (1)

0

sitasahau nilipolala na mwanamke juu ya kaburi

NILIISHI maisha ya starehe. Ujana ulinikamata vilivyo. Pombe na wanawake havikunipita, walionifahamu waliniita ‘popo.’ Nilikuwa popo kweli, popo kasoro mabawa!

 

Mchana nilifanya kazi ili nipate masurufu ya kwenda kutesa katika viwanja. Japo nilifanya kazi za kijungujiko, fuko langu halikukauka fedha, hata bila aibu ya ule umri wangu wa miaka 33 na sura iliyokomazwa na ulevi, nilipenda kujiita tajiri mtoto!

 

Jumamosi usiku nilikwishamaliza kuvalia mavazi ya kupendeza. Nilijitazama katika kioo, nikaiona fulana yangu nyeusi na jinsi ya bluu, shingoni nilijaza cheni nyingi hata nikafanana na mbuzi mgeni. Haraka nilivaa viatu vyeupe, nikatoka ndani, nikafunga mlango kisha nikapaza sauti, “nakula ujana nitapumzika nikiwa babuuuu!”

 

Wapangaji wenzangu waliyazoea makelele yangu. Niliwasikia wakicheka ndani ya vyumba vyao. Kichwa maji mimi, nikapayuka tena, “laleni hamna hela.” Jirani mmoja aliyekerwa na kauli hiyo, akajibu kwa sauti kubwa kuliko yangu, “ungekuwa na hela ungenunua kitanda paka wewe!”  Kauli hii ikaamsha vicheko vingi zaidi. Kupunguza hasira na aibu, nikaporomosha tusi kali la nguoni lililozua ukimya. Kisha huyoo, nikaenda kusaka vimwana na vilevi.

 

Nilifika katika baa moja iliyojaaliwa wahudumu warembo. Nikavuta kiti kwenye meza. Nikaletewa bia bila kuagiza, walinifahamu. Nilipiga mafunda saba, akili ikachangamka. Basi nikawa napiga mafunda kadhaa, huku nasikiliza muziki mororo.

 

Nilikunywa tani nyingi za bia. Akili yangu ikapumzika kwa muda, pombe ikashika usukani. Kichwani niliwaza kupata mwanamke wa kulala naye. Sikumtaka mwenye maadili, asingekubali kuishi na mlevi kama mimi.  Nilitaka ‘kahaba’, tuwe wapenzi kwa sekunde kadhaa, nimpe fedha tuachane kwa amani.

 

Nilipotoka nje sikupata shida ya kuwaita vimwana, kama mbu, walikuja wenyewe. Wote hawa walikosa cha kuuza, wakaamua kuuza miili yao. Nilipochoka kuwasikiliza wakijinadi, nikaamua kusema, “leo nataka rangi ya kunde! Awe na mzigo, sifa nyama, mzoefu wa kutoa ‘saidoni’ atapewa kipaumbele.”

 

Nilimpata kimwana mmoja aliyekuwa na sifa nilizotaka. Tukaanza kuelewana:

 

“Utanifanyia shilingi ngapi leo?” niliuliza kilevi.

“Buku mbili tu… vitu vimepanda bei.”

Sikutaka kuzungumza zaidi, nikakubaliana naye huku tukiongozana kuelekea eneo la kumaliza biashara yetu. Makaburini.

 

Itaendelea kesho…

 

Leave A Reply