The House of Favourite Newspapers

Vai: Pombe Ndio Tulizo La Mawazo Yangu!

1
Msanii wa filamu, Isabela Francis maarufu kama Vai wa Ukweli, anayeishi Vatican- Sinza, jijini Dar akiandaa viungo vya mboga.

 

KARIBU mpendwa msomaji wa Mpaka Home, kama ilivyo kawaida ya kila wiki, safu hii inakuletea maisha halisi wanayoishi mastaa wa fani mbalimbali Bongo nje ya kazi zao.

Wiki hii tumetembelea nyumbani kwa msanii wa filamu, Isabela Francis maarufu kama Vai wa Ukweli, anayeishi Vatican- Sinza, jijini Dar. Ungana nami hapa chini uweze kujua mengi kuhusu yeye.

Mpaka Home: Mambo vipi Vai, naona uko bize na usafi, nilijua utakuwa na dada wa kazi!

…Akiweka sawa meza yake ya TV.

Vai: Hapana, msichana wa nini, kazi ndogondogo kama hizi lazima mwanamke azifanye na wala sina mzuka wa kumuajiri mtu.

Mpaka Home: Kitu gani cha kwanza kufanya ukiamka?

Vai: Kwanza napenda kuweka mwili wangu safi, kisha ndiyo kazi nyingine zinafuata.

Mpaka Home: Kuhusu kifungua kinywa, unapendelea nini na mchana je?

Vai: Sipendi chai, hivyo kifungua kinywa changu ni pombe na mchana napenda sana kula maini.

Mpaka Home: Hapa nyumbani unaishi na nani?

Vai: Ninaishi peke yangu tu.

Mpaka Home: Vipi kuhusu yule mchumba uliyekuwa unaishi naye, akakuvalisha na pete ya uchumba?

Vai: Ni kweli nilikuwa naye, lakini nimeshaachana naye kitambo, kwa sasa niko singo.

…Akiendelea kuandaa mazagazaga ya kupika.

Mpaka Home: Kitu gani unachopenda kiwepo nyumbani kwako na hakipo?

Vai: Natamani sana ningekuwa na baa ya vinywaji vya kila aina.

Mpaka Home: Kipindi cha nyuma ulikuwa ukipenda sana kutumia vilevi, vipi kwa sasa hali ikoje?

…Akianika nguo.

Vai: Bado napenda, pombe ndiyo tulizo la mawazo yangu, siku nikiwa sina hela ndiyo navumilia kwelikweli.

Mpaka Home: Mastaa wengi kwa sasa wana watoto, vipi wewe?

Vai: Sifuati mkumbo, maana maisha yangu mwenyewe siyaelewi kabisa, niongeze tena mtoto? Nitampa shida tu.

…Akipiga deki

Mpaka Home: Unahamahama sana nyumba unazokaa, nini tatizo?

Vai: Mimi sina tatizo, labda nyumba ninazopata ndiyo tatizo.

Mpaka Home: Nakushukuru sana Vai kwa ushirikiano wako.

Vai: Ahsante, karibu tena.

MPAKA HOME: IMELDA MTEMA | RISASI JUMAMOSI 

WASTARA AMKUMBUKA MAREHEMU SAJUKI, ANATAMANI KUMPATA KAMA YEYE!

1 Comment
  1. […] tani nyingi za bia. Akili yangu ikapumzika kwa muda, pombe ikashika usukani. Kichwani niliwaza kupata mwanamke wa kulala naye. Sikumtaka mwenye maadili, […]

Leave A Reply