The House of Favourite Newspapers

Stars Yatoshana Nguvu Na Madagascar, DR Congo Waongoza Kundi

0

TIMU ya taifa ya Tanzania leo Novemba 14 imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Madagascar kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia.

 

Mchezo wa leo ulikuwa ni kuhitimisha ndani ya kundi J ambapo alikuwa anatafutwa mshindi kati ya Benin na DR Congo kuweza kutinga hatua ya mtoano na mwisho ni DR Congo wameibuka wababe kutoka kundi hili ambalo Tanzania iliwahi kupata nafasi ya kuongoza kwa muda.

Kipindi cha kwanza kwenye mchezo wa leo Stars iliweza kucheza kwa kujiamini na ilipata bao kali dakika ya 23 kupitia Simon Msuva.

Hakim Abdalah huyu alikuwa mtibua mipango baada ya kupachika bao la kusawazisha dakika ya 74 kwenye mchezo huo ambao ulikuwa na mashabiki kama wote wa Madagascar.

 

Sare hiyo inaifanya Tanzania kumaliza ikiwa nafasi ya tatu kwenye kundi J na pointi zake ni 8 huku DRC Congo ikiwa imefuzu hatua ya mtoano na pointi 11 baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Benin.

Nahodha Mbwana Samatta pamoja na kipa Metacha Mnata hawakupata nafasi ya kuanza baada ya kuwekwa karantini kwa kile kilichoelezwa kwamba wana Corona.

Leave A Reply