×

Vibonge Yanga Waandaliwa Dozi

DAKTARI wa Yanga, Shecky Mngazija, amesema wachezaji wa timu hiyo walioongezeka uzito na kuwa vibonge wameandaliwa dozi nzito ya mazoezi itakayokuwa kila siku asubuhi na jioni ili kurudi kama zamani.

 

Mngazija amesema ameandaa programu kwa wachezaji watatu ambao baada ya kufanyiwa vipimo wamebainika kuongezeka uzito kuliko kawaida, hivyo lazima wapambane kurudisha miili yao katika utimamu unaotakiwa kabla ya ligi kuendelea Juni 13, mwaka huu.

 

Hivi karibuni wakati timu zimeruhusiwa kuanza mazoezi, Yanga iliwafanyia vipimo mbalimbali wachezaji wake ikiwemo ishu ya uzito na taarifa zinaeleza kuwa David Molinga Patrick Sibomana na Yikpe Gislain Gnamien wameongezeka uzito.

 

Mngazija alisema: “Wapo baadhi ya wachezaji ambao tumewafanyia vipimo na tumewabaini kuwa na ongezeko la uzito kidogo, hivyo tumeandaa programu maalumu kwa ajili ya kuwaweka sawa na watatakiwa kufanya mazoezi kila siku asubuhi na jioni hadi warudi kwenye hali zao za kawaida.”

Stori: ISSA LIPONDADar es Salaam

Leave a Comment