Straika Mnyarwanda: Nataka Kucheza na Tshishimbi na Ajibu

BAADA ya juzi kusaini mkataba wa miaka miwili ya kuichezea Yanga, kiungo mshambuliaji mpya Mnyarwanda, Issa Bigirimana ‘Walcott’ amemuulizia Ibrahim Ajibu akitaka kujua anabaki au anaondoka Jangwani.

 

Bigirimana alisaini mkataba huo juzi baada ya kufi kia makubaliano mazuri na viongozi wa Yanga kabla ya kumpa mkataba huo akitokea APR ya Rwanda aliyokuwa anaichezea.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Bigirimana alisema kuwa, anavutiwa na wachezaji wengi Yanga, lakini zaidi ni Ajibu ambaye alimmwagia sifa nyingi kuwa ni mchezaji anayemkubali kutokana na kiwango kikubwa alichokuwa nacho.

 

“Wapo wachezaji wengi ninaowakubali Yanga lakini huyu jamaa anayevalia jezi namba 10 (Ajibu) anajua sana na ningefurahi kuona ninacheza naye timu moja kwenye msimu ujao.

 

“Mwingine ni Tshishimbi yule kiungo mwenye rasta, ninampenda sana anacheza kwa kutumia akili nyingi na ufundi mwingi, ninaamini nikicheza naye pamoja tutatengeneza kitu kizuri ndani ya Yanga,” alisema Bigirimana.

Wilbert Molandi, Dar es Salaam

Loading...

Toa comment