The House of Favourite Newspapers

Super Nyamwela: Siachi Kunengua, Mwili Unaruhusu

MNENGUAJI wa kitambo katika Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Musa Hassan ‘Super Nyamwela’ amesema kuwa, pamoja na kudumu kwa muda mrefu kwenye fani hiyo, lakini hana mawazo ya kuiacha kwa sababu bado mwili unamruhusu.

 

Akizungumza na Over Ze Weekend, Nyamwela alisema ana watoto wakubwa sasa ambao aliwazaa akiwa ananengua, lakini itakuwa ngumu kuiacha kazi hiyo kwa sababu ipo kwenye damu na anataka aache historia kutokana na kazi yake hiyo.

 

“Sijafikiria kabisa kuacha unenguaji ambao nimeanza mwaka 1991, lakini kikubwa mwili wangu unaruhusu kabisa kufanya ninachofanya na hata watoto wangu wanaheshimu kazi yangu, ninataka niweke historia kwa kazi yangu hii,” alisema Super Nyamwela ambaye ni mnenguaji mahiri wa bendi hiyo.

IMELDA MTEMA

Comments are closed.