Stori: Musa Mateja
Juzikati yaliibuka madai kuwa msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Baraka da Prince alizaa na binti mmoja aitwaye Candy anayetokea Iringa lakini akawa hatoi matunzo kwa mtoto ikiwa ni pamoja na kumpotezea mzazi mwenzake huyo.
“Tatizo sasa hatoi huduma ya mtoto, yaani kila siku nikimpigia simu yuko bize anadai yuko studio na huku nyumbani kwetu wananifukuza,” alilalama Candy.
Akizungumzia tuhuma hizo, Baraka amesema anakiri kuwa ana mtoto lakini ameshangazwa na kuumizwa sana na malalamiko hayo.
“Naanzaje kutelekeza mtoto? Hayo madai hayana ukweli, ngoja nione jinsi ya kudili la suala hili,” alisema msanii huyo anayefanya poa kwenye game kwa sasa.