visa

TANSHA ATAJA SABABU ZA KUITOSA WCB

W AKATI ngoma yake ikiwa ‘hot’ katika redio mbalimbali nchini Kenya, demu wa staa wa Bongo Fleva, Tanasha Donna Oketch ametaja sababu ya kuitosa lebo ya kurekodi muziki ya Wasafi  Classic Baby ‘WCB’. Tanasha anayetikisa na Ngoma ya Radio akiwa amemshirikisha msanii kutoka nchini kwao, Baraka Jacuzzi alisema hayo kwenye mahojiano na Switch TV. Alisema, japo yupo karibu na Diamond lakini hana mpango wa kuingia katika studio zake (Wasafi  Record) kurekodi ngoma.

“Nafi kiri aina ya muziki ninayoifanya ipo tofauti sana na Wasafi  Record. Labda kama Diamond ataanzisha Wasafi  Caribbean au Hip Hop hapo naweza lakini kwa sasa siwezi,” alisema Tanasha. Ngoma ya Tanasha imepikwa katika studio mbalimballi nchini Kenya huku video ikishutiwa na Direkta Ivan Odie wa nchini humo
Toa comment