The House of Favourite Newspapers

Timbwili Laibuka kwenye mazishi ya mwendesha bodaboda, Gidion Sanaa ‘Bakhresa’ wa Tabata- Video

0

Timbwili limeibuka kwenye mazishi ya mwendesha bodaboda, Gidion Sanaa almaarufu Bakhresa wa Tabata ambaye aliuawa kikatili kwa kupigwa na kuchomwa moto akituhumiwa kuiba betri za pikipiki ambapo wananchi wamegomea kumzika wakitaka waliohusika na mauaji hayo wakamatwe.

Tukio hilo likasababisha Jeshi la Polisi kuingilia kati kutuliza vuguvugu lililokuwa linazidi kuongezeka.

Hatimaye mwili wa Bakhresa ukazikwa majira ya saa kumi jioni kwenye Makaburi ya Vingunguti Machinjioni chini ya ulinzi mkali.

Bakhresa aliuawa usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita, akituhumiwa kwa wizi, madai ambayo ndugu, majirani na watu wanaomjua kukanusha vikali wakieleza kwamba hakuwa mwizi.

Leave A Reply