Tshabalala Aiwekea Ngumu Simba

LICHA ya uongozi wa Simba kumuita mezani beki wake Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ kwa ajili ya mazungumzo ya mkataba mpya meneja wa nyota huyo amefunguka kuwa wanaangalia na upepo wa Afcon unaenda vipi kutokana na ubora wa mchezaji wake.

 

Tshabalala ni mmoja kati ya wachezaji ambao mikataba yao imemalizika pamoja na Haruna Niyonzima, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Aishi Manula na Said Mohammed. Harry Chibakasa ambaye ni meneja wa beki huyo alisema;

 

“uongozi wa Simba tayari umetuita mezani kwa ajili ya mazungumzo ya mkataba mpya hilo halina tatizo kwa sasa pia tunangaalia kule Afcon mambo yanakwendaje kwanza hivyo tutachelewa kidogo.”

“Sababu Tshabalala ni mchezaji mwenye mafanikio kwa sasa ambapo ametoa mchango mkubwa kwa timu yake kutwaa ubingwa mara mbili jambo ambalo sio dogo na linatakiwa kuangaliwa kwa umakini mkubwa kabisa,”alisisitiza.

ALI KIBA “NILIKUA Natamani ABDU KIBA Afunge MZUKA”

Loading...

Toa comment