Tshishimbi Atamba, Kisa Sibomana

KIUNGO mkabaji wa Yanga Mkongomani, Papy Tshishimbi amekiangalia kikosi kipya cha timu hiyo na kutamka kuwa msimu huu utakuwa mzuri kwao wa kuchukua makombe yote watakayoshindana kutokana na usajili bora uliofanywa na mabosi wake.

Wachezaji baadhi waliosajiliwa na Yanga ni Patrick Sibomana, Lamine Moro, Juma Balinya, Sadney Urikhob, Moustafa Selemani, Farouk Shikalo na Muharami Issa ‘Marcelo’.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Tshishimbi alisema kuwa wana kila sababu ya kufanya vema kwenye msimu ujao kutokana na ubora wa kikosi tofauti na cha msimu uliopita.

Tshishimbi alisema kuwa licha ya ubora wa kikosi chao, bado kinahitaji marekebisho madogo ambayo kocha wao Mwinyi Zahera ameyaona na anaendelea kuyafanyia kazi.

 

“Kila mtu amekiona kikosi chetu kipya, ninaamini kuwa wameridhishwa na ubora wa timu ambayo haimtegemei mchezaji tofauti na msimu uliopita ambao ulikuwa mgumu kwetu.

 

“Lakini msimu huu utaona kikosi chetu kimekamilika kila sehemu kwa maana kila nafasi ina mchezaji zaidi ya mmoja, kama siku akikosekana mchezaji mmoja kwa kadi au majeruhi basi yupo mwingine bora.

 

“Hivyo, mashabiki wa Yanga warejeshe matumaini kwenye timu hiyo katika kuelekea msimu ujao, na zaidi niwaombe wajitokeze kwa wingi uwanjani kwa ajili ya kutusapoti,” alisema Tshishimbi.


Loading...

Toa comment