testiingg
The House of Favourite Newspapers

Uwanja Wa Amaan Zanzibar Wakaguliwa Maandalizi Ya AFCON 2027

0

Timu ya Wakaguzi ya utayari wa nchi za Kenya, Uganda na Tanzania kuhusu utayari wao wa kuwa wenyeji AFCON 2027, leo hii Julai 31, 2023 wako Zanzibar ambapo wamekagua Uwanja wa Amaan, hospitali ya Mnazi Moja, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume pamoja na viwanja vingine vya mazoezi.

Timu hiyo kutoka Shirikisho la Mpira Afrika (CAF) imezungukia maeneo hayo ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)  Wallace Karia na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar  (ZFF) Bw Suleiman Mahamud Jabir.

Maafisa wengine kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwemo Kaimu Mkurugenzi wa Michezo Bw. Ally Mayayi na Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha na kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni Kamishna Idara ya Michezo Bw, Ameir Mohammed, Katibu Mtendaji Baraza la Michezo Zanzibar Saidi Marine pamoja na maafisa wengine kutoka TFF na ZFF walikuwa sehemu ya walioungana na wataalamu kutoka shirikisho la soka Africa  CAF kuukagua Uwanja wa Amaan.

Leave A Reply