The House of Favourite Newspapers

Uwanja Wa Ndege JNIA Terminal 2 Kufungwa Kwa Muda Kupisha Maboresho 2024

0

Naibu waziri wa Uchukuzi David Kihenzile amesema Uongozi wa uwanja wa ndege wa kimataiafa wa Julius Nyerere – Terminal 2 unatarajiwa kufanyiwa mamboresho makubwa mwaka 2024 ambapo yatapelekea kufungwa kwa muda kwa uwanja huo ili kufanya maboreeho hayo.

Kihenzile ameyasema hauo alipokuwa Jijini Dar es Salaam akiendelea na ziara yake ya siku mbili ya kukagua kwa lengo la kujuonea namna shughuli zinavyoendela katika uwanja huo.

Kihenzile amesema iwapo wananchi wataona uwanja huo umefungwa wasishtushwe au kupotoshwa wajue kuwa ni ukarabati huo umeanza na utakamilika kwa upesi ili shughuli zake ziendelee.

Vilevile Kihenzile amesema mamboresho hayo ni kutokana na juhudi za Serikali za kuuongeza uwanja huo uwezo wa kuhudumia abiria wengi zaidi kwani jitihada za Rais Dkt. Samia suluhu Hassan za kuitangaza nchi kupitia filamu ya Tanzania the Royal Tour zimezaa matunda yanayopelekea uhitaji wa kupanua uwanja hio.

Kwa upande mwingine Kihenzile amesema ameridhishwa na jitihada zinazofanya na uongozi huo za kuhakikisha ndege na abiria ni salama na kusisitiza kuwa katika jambo muhimu kwenye uwanja wa ndege ni usalama wa abiria, mizigo yao na ndege yenyewe.

Leave A Reply