Uwoya Gusa Unate!
Imewekwa na on February 17th, 2017 , 07:08:00pm

Uwoya ni Gusa Unate!

Irene Uwoya

Na IMELDA MTEMA| GAZETI LA IJUMAA| HABARI

DAR ES SALAAM: Msanii maarufu wa filamu Bongo, Irene Uwoya (pichani)  anatajwa kuwa kati ya mastaa wa kike Bongo aliyewahi kutoka na mastaa na vigogo mbalimbali huku ikidaiwa kuwa, kila aliyekuwa naye alimuacha yeye na si kuachwa. Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Uwoya aliyeomba hifadhi ya jila lake, staa huyo mwenye shepu na mvuto wa kudatisha kimahaba amekuwa akipapatikiwa sana na wan aume lakini mwisho wa siku huishia kuwaliza kwani yeye ndiye anayeamua kuendelea na wewe au akuache.

“Uwoya namjua vizuri sana, yule ni hatari kwa wanaume. Kwanza anajijua kuwa ni mzuri hivyo amekuwa akiwadenguliwa wanaume wengi sana na orodha ya wanaomtokea kila siku ni kubwa.

“Lakini akitokea kukupenda atakupenda kweli hadi unaweza kuona kero. Kwa kifupi anajua kupenda, kujali na kubembeleza kiasi kwamba ukinasa kwake ni vigumu kutoka ndiyo maana wapo wanaosema kwamba, Uwoya ni gusa unate!

Irene Uwoya

“Ila sasa, anaweza kukuchanganya kwa mahaba mazito lakini siku akiamua kukuacha, anakuacha na si mtu anayependa sana kudumu na mwanaume mmoja kwa muda mrefu, fuatilia utagundua hili.

UWOYA ALIWAHI KUKIRI HILO

Katika moja ya mazungumzo na mwandishi wetu, staa huyo aliwahi kukiri kuwa, hapendi kugandwa sana na mwanaume mmoja kwa muda mrefu. “Yaani mimi kukaa muda mrefu na mwanaume sipendagi kabisa na sina mzuka huo. Ndiyo maana mtu nikiamua kumbwaga anahaha na wengine watabembeleza weee lakini wala sina tabia ya kurudi nyuma, kwa kifupi sipendi kudumu na mpenzi,” aliwahi kusema Uwoya.

KUMBUKUMBU ZINAONGEA

Hata hivyo, kumbukumbu zinaonesha kuwa, wanaume wengi waliowahi kutoka na staa huyo ukiacha mumewe, Hamad Ndikumana ambaye alionekana kufa na kuoza kwake kiasi kwamba hakukubali kirahisi kuachwa, wengi wao walioonja penzi lake ilikuwa vigumu kutoka hadi walipoachwa.

UWOYA ANASEMAJE?

Kufuatia ripoti hiyo, mwandishi wetu alimtafuta Uwoya ili kuzungumzia siri ya kugandwa na wanaume hadi kufikia hatua ya kuitwa gusa unate ambapo alikuwa na haya ya kusema: “Kwanza ujue mimi ni mwanamke ambaye sipapatikii mwanaume, anayetokea na kuonesha kunipenda, nikazungumza na moyo wangu ukakubali kumpa nafasi, namkubalia lakini ujue siku moyo wangu ukisema basi, hakuna mjadala, nakuacha. “Lakini lingine ni kwamba, moja ya sifa ya mwanamke ni kujua kumshika mwanaume, kwamba akiwa na wewe ujue kumfanya asifikirie kukuacha, ufanye kila unaloweza anase kwako, kwa hiyo utundu na ubunifu ndiyo siri yangu.”

HISTORIA YAKE!

Uwoya katika maisha yake ya kimapenzi amewahi kutoka kwa siri na vigogo pamoja na mastaa mbalimbali akiwemo pedeshee mmoja aliyekuwa akifahamika kwa jina la Ababuu, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Hamis Baba ‘H-Baba’, Jovann Msami na wengineo.

 

Kwa stori zote kali, Tu-follow

Facebook @Globalpublishers

Twitter @GlobalHabari

Instagram @GlobalPublishers

YouTube @GlobalTVTZ

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Stori zinazo husiana na ulizosoma