KIKOSI cha Yanga kimewasili jijini Dar es Salaam kikitokea jijini Mwanza ambapo waliweka kambi kwaajili ya kujiandaa na mechi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ambayo itapigwa Septemba 14 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kocha Zahera amesema wamejindaa vizuri kuikabili Zesco huku mchezaji ambaye aliweza kuifungia Yanga mabao 3 katika mechi za kirafiki walizocheza Yanga dhidi ya Pamba na Toto Afrika David Molinga maarufu Falcao atakosekana katika mechi hiyo kutokana na kutokamilisha leseni yake.