Wakala wa Beki Ivory Coast Akutana na Mabosi wa Simba

KWENYE ripoti ya usajili wa Simba ambayo imeachwa na kocha wao Patrick Aussems, amewataka vigogo hao kusajili beki mmoja wa kati kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, sasa Jumamosi iliyopita mabosi wa Simba walikutana na wakala Patrick Gakumba kwa ajili ya kumalizana kuhusiana na beki Ange Baresi Gloudoueu ambaye ni raia wa Ivory Coast.

 

Mabosi hao wa Simba walikutana na Gakumba ambaye yupo nchini na akiwa amefikia kwenye moja ya hoteli zilizopo Kariakoo kwa ajili ya kumsajili Gloudoueu ambaye ana uzoefu mkubwa na michuano ya kimataifa.

 

Beki huyo ambaye kwa sasa anakipiga ndani ya Asec Mimosas ya Ivory Coast, anapigiwa hesabu kali na Simba ili kuja kuongeza

nguvu katika kikosi hicho kwa ajili ya michuano ya kimataifa.

 

Taarifa za ndani ambazo Championi Jumatatu, limezipata ni kwamba mabosi wa Simba walikutana na Gakumba juzi Jumamosi na kuzungumza namna ya kumalizana na Gloudoueu.

 

“Ndiyo ni kweli, viongozi wa Simba na Gakumba walikutana juzi (Jumamosi) na kuzungumza naye.

 

“Mabosi hao wakiongozwa na Mtendaji Mkuu (Crescentius Magori) walizungumza naye juu ya usajili huo na muda siyo mrefu huenda beki huyo sambamba na wachezaji wengine watatu wakaja Simba kwa ajili ya kumalizana na uongozi,” kilisema chanzo hicho.

 

Ikumbukwe kuwa Gakumba ndiye ambaye amemleta nchini straika Meddie Kagere kutoka Gor Mahia na kumsainisha mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo.

Sweetbert Lukonge na Said Ally, Dar

TAZAMA MBWANA SAMATTA Alivyotunukiwa TUZO ya Heshima na GLOBAL GROUP


Loading...

Toa comment