The House of Favourite Newspapers

Wanaume Jiandaeni Kudungwa Sindano na Dk Sasha.

Kweli ujana ni maji ya moto; unaweza ukakufanya ukadharaulika na kuonekana mtu wa hovyo lakini ukitulia na kuamua kuwa msomi unaweza kufanya mambo makubwa watu wakashangaa na ukapata heshima.  Hilo limejidhihirisha kwa mrembo Sasha Kassim ambaye ameingia katika Chuo cha Udaktari Bungando mkoani Mwanza kusomea udaktari. Kabla ya kujitupa kwenye fani hiyo, mrembo huyo alikuwa gumzo kwa mapichapicha ya ajabu mitandaoni huku shepu yake ya kujaajaa ikitolewa macho sana na wanaume wakware.

Sasa basi, Sasha ameamua kuwa daktari na anasema wanaume jiandaeni kuchomwa sindano za kutosha pale mtakapokutana naye hospitalini. Awali, Wabongo wengi walikuwa wakimsema vibaya video queen lakini mwisho wa siku mwenyewe aliamua kuingia darasani, sasa anatarajia kuwa daktari. Mrembo huyu amefanya mahojiano na Showbiz Xtra ambapo alifunguka mambo kibao;

Showbiz: Sasha umepotea Jiji la Dar es Salaam uko wapi kwa sasa na unafanya nini?

Sasha: Kwa sasa nakaa Mwanza nasomea udaktari Bugando.

Showbiz: Sasha wewe wewe! Unasomea udaktari si maajabu hayo daktari utakuwa wewe uliyekuwa ukishinda mitandaoni na picha zako za kuonesha shepu lako itakuwaje.

Sasha: Wewe utashangaa lakini mimi huyu ninasoma kwa miaka mitatu, nimeshakata mmoja ninasoma na nina malengo makubwa sana kwani nitakuwa na maabara yangu kubwa ambayo itahudumia watu wengi.

Showbiz: Uliwahi kusema hupatikani na wanaume wa Kibongo itakuwaje kwenye kuwahudumia.

Sasha: Hahahaha nicheke kwa sauti mimi, nitakutana nao chumba cha sindano wakae tayari nitaanza kwa kuwadunga sindano wao kwa sababu walinikejeli sana na kuniita majina mabaya kisa tu ni mapichapicha.

Showbiz: Unatisha Sasha kwa hiyo wewe unasomea udaktari kisha ukawadunge wanaume sindano ni madaktari wachache hufanya yote, sindano mimi najua wanachoma manesi tu.

Sasha: Mh! Udaktari wangu utakuwa ni wa kujitolea sana pale mgonjwa atakaponihitaji hata sindano nitachoma sina shida hivyo ninachosema ninamaanisha wala si utani.

Showbiz: Nani alikushawishi kurudi shule tena ukahama kabisa Dar.

Sasha: Unajua nilirudi shule baada ya kurejea kwa mama yangu ambaye anakaa Mwanza, mwanzo nilikuwa na utoto sana, sasa hivi nimekuwa nimeona nilikokuwa hapakuwa sawa.

Showbiz: Katika matukio uliyowahi kufanya kabla hujaingia kwenye udaktari ni yapi unayajutia hutamani kuyakumbuka?

Sasha: Sijutii chochote kwa sababu naamini ni utoto huo na kila mtu huwa anapitia halafu mimi sina kitu kibaya sana nilichokifanya ambacho kitanifanya nijutie.

Showbiz: Umekuwa ukionekana kupiga picha kwenye magari mawili tofauti je, ni ya kwako na umepataje?

Sasha: Yaah ni ya kwangu, kabla ya kupewa na mpenzi wangu lingine la kwanza kabisa nilipewa na mama yangu niwe natumia tumia.

Showbiz: Umesema una mpenzi na amekuhonga gari je unatarajia kuolewa lini?

Sasha: Nisiwe muongo kwenye suala la ndoa hatujafikia huko na kwa sababu bado ninasoma naona kama litakuwa ni suala la mwisho kabisa.

Showbiz: Huko chuo huwa hupati usumbufu wa wanachuo wenzako kutokana na jinsi ulivyo?

Sasha: Usumbufu napata kama kawaida kwa sababu hata isingekuwa shepu wangenisumbua tu hivyo mara nyingi huwa napenda kuvaa hijabu na nikabu kuepusha hilo lakini niwapo nje ya darasa, sio darasani

 

Comments are closed.