WARENO KUINUFAISHA SIMBA SC

KAMA zali vile! Simba i tanufaika na maufundi ya Wareno ambapo anatokea staa mkubwa wa soka duniani, Cristiano Ronaldo anayekipiga Juventus ya Italia.

 

Hii ni baada ya Mwekezaji wa Simba, Mohammed Dewji kuitembelea FC Porto ya nchini Ureno na kujifunza masuala tofauti ya kisoka. FC Porto inashiriki Ligi Kuu ya Ureno na ndiyo mabingwa mara nyingi katika ligi ya kwao na sasa wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo.

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, juzi Jumanne Mo aliandika maneno haya ambayo yana faida kubwa kwa soka la Tanzania.

 

“Jana nilipata nafasi nzuri ya kujifunza nilipoitembelea FC Porto ambapo niliweza kujua fursa za ushirikiano kwa kituo cha kukuzia vipaji cha Simba huko mbeleni. “Tuna mengi ya kujifunza na kupata kutokana na uzoefu wa Porto FC. Natarajia kuimarisha mazungumzo yetu hivi karibuni.”

Na:WILBERT MOLANDI,

Toa comment