The House of Favourite Newspapers

Wazadi Wagomea Shule Kufundisha Kingereza

0

WAZAZI wa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mukendo, iliyopo Musoma mkoani Mara wamekataa mpango wa Serikali kubadili Shule hiyo ili iwe Shule ya Mkoa yenye Mkondo wa Kiingereza.

Mwenyekiti wa Kamati ya Wazazi katika Shule hiyo, Moshi Faraji amesema awali walikubali kwa kutoa masharti lakini sasa wamebadilika, hawataki kabisa.

“Walitaka wanafunzi wa Kiingereza waanze kuandikishwa kadri waliopo wanavyomaliza la Saba lakini Novemba tukaambiwa hiyo haiwezekani, lazima wanafunzi waliopo waondolewe wote na hapo shida ndipo ilipoanzia,” amesema Faraji.

Licha ya mazungumza baina yake na uongozi wa Manispaa hiyo kufikia muafaka wa wanafunzi pamoja na walimu wao kuhamishiwa Shule ya Msingi Iringo, wazazi wenzake wameshikilia msimamo wa kutotaka mabadiliko hao.

Leave A Reply