ALHAMISI ijayo, katika Viwanja vya Mbagala Zakhem kuanzia mapema, shughuli kubwa kuwahi kutokea katika Tanzania, zitaanza ambazo mwishowe, mtu mmoja, ambaye ni msomaji wa magazeti ya Global Publishers, atatangazwa kuwa mshindi wa droo kubwa ya Shinda Nyumba yenye thamani ya mamilioni ya shilingi.
Shughuli hiyo, itakayofanywa mbele ya maofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, itahitimisha safari ndefu na ngumu ya miezi sita, ambayo wasomaji wa Magazeti ya Risasi, Amani, Uwazi, Championi, Ijumaa Wikienda na Ijumaa walianza kujipatia kuponi, huku pia wakijishindia zawadi nyingi ndogondogo, zikiwemo pikipiki, televisheni za kisasa, vyombo vya nyumbani na ving’amuzi.
Kuponi ya ushindi bado ni siri aijuaye Mungu, kwa maana hiyo wanunuzi wa magazeti ya wiki hii bado wana nafasi kubwa ya kuibuka washindi. Hujachelewa, nenda kanunue sasa nakala ya gazeti uwe mmoja wa wamiliki wa nyumba ya kisasa, yenye samani ndani yake, iliyopo Salasala, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Ni rahisi kuipata nyumba hii, ukinunua moja ya magazeti hayo kwa shilingi mia tano tu (isipokuwa Ijumaa linalotoka siku ya Ijumaa linalouzwa buku), kata kuponi iliyopo katika ukurasa wa pili, halafu ijaze kama ilivyoelekezwa na baada ya hapo, mtafute wakala wa magazeti ya Global Publishers mpatie au kama uko Dar, nenda moja kwa moja ofisini kwetu, Bamaga, Mwenge.
Zipo simulizi nyingi zinazoonesha jinsi watu wengi walivyoweza kupata vitu vyenye thamani kubwa kwa kushiriki michezo ya kubahatisha kama hii, kwani unaweza kuona kama kitu kisichowezekana au kimepagwa, lakini ukweli ni kuwa wewe unayesoma hapa, unaweza kuibuka mshindi.
Mtu anapata kitu katika kujaribu, huwezi kufanikiwa chochote katika maisha bila kujaribu, ndivyo ambavyo wafanya-biashara wakubwa walivyofanya, walianza kufanya na hatimaye wakafanikiwa. Hata waliofanikiwa kupitia kilimo, walianza kwa kulima.
Huwezi kuwa mshindi wa nyumba hii kama hutajaribu kujaza kuponi na kutuma. Na ukituma nyingi zaidi unakuwa katika nafasi kubwa zaidi ya kuibuka mshindi.

