The House of Favourite Newspapers

Waziri Shonza mgeni rasmi Siku ya Urembo wa Asili

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza.

WAKATI siku zikiwa zinakaribia kufikia Siku ya Urembo wa Asili, (Julai 27 na 28 katika Viwanja vya Life Park, Mwenge jijini Dar) habari ikufikie kuwa mgeni rasmi katika siku hiyo atakuwa ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza.

 

Akizungumza na Star Showbiz, mratibu wa tamasha hilo lenye kauli mbiu ya Nywele za Asili Siyo Ushamba ni Ujanja, Antu Mandoza aliwaomba wajasiriamali na wadau wa urembo kujitokeza kwa wingi kwani hakutakuwa na kiingilio.

 

“Kutakuwa na vitu vingi sana kama vile upimaji wa kansa, wajasi-riamali na wakufunzi wa masuala ya urembo ambao siku hiyo watafundisha kutengeneza baadhi ya vitu live kama vile Showergel.

 

“Kwa hiyo kama unajijua ni mjasiriamali wa mambo ya ngozi, nywele, ni msusi hii ni fursa kubwa sana kwako kwani siku hiyo mbali na kuuza vipodozi, wahudhuriaji watapata fursa ya kujifunza urembo wa asili kupitia kwa madaktari wetu na timu ya ushauri,” alisema Antu Mandoza

Comments are closed.