The House of Favourite Newspapers
gunners X

Waziri Simbachawene Awapongeza Askari kwa Kulinda Amani Kufuatia Fununu za Maandamano – Video

0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, ametoa pongezi kwa askari wa vikosi vya ulinzi na usalama kwa kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kutawala nchini, kufuatia fununu zilizokuwepo za maandamano yasiyo na kikomo.

Waziri Simbachawene alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam baada ya kukutana na askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na wale wa Jeshi la Polisi katika mitaa mbalimbali ya jiji hilo. Amesema askari wamefanya kazi kubwa na kwa weledi katika kulinda usalama wa wananchi na mali zao, hatua iliyosaidia kuzuia hofu na kuruhusu shughuli za kiuchumi kuendelea kama kawaida.

Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kuviwezesha vyombo vya ulinzi na usalama ili viendelee kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, huku akiwataka wananchi kuendeleza ushirikiano na kutoa taarifa pale wanapoona viashiria vya uvunjifu wa amani.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by globalpublishers (@globaltvonline)

Leave A Reply