The House of Favourite Newspapers

Yanga Yapania heshima tu Kwa Azam

HUKU wakibakiwa na mchezo mmoja dhidi ya Azam, uongozi mpya wa Yanga chini ya Mwenyekiti Mshindo Msolla umekutana na wachezaji pamoja na benchi la ufundi na kumaliza matatizo yote.

 

Akizungumza na Spoti Xtra Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema kuwa “Kwanza cha msingi tumekubaliana na wachezaji kwamba tunatakiwa tumalize ligi kwa heshima kwani hapa katikati wengi mnajua kuwa tulikuwa na matatizo ambayo yametupelekea tushike nafasi ya pili.”

 

“Kwani tulikuwa na matatizo yetu likiwemo suala zima la kifedha pamoja na changamoto zingine tulizokutana nazo uwanjani ambazo wengi mnazijua kwa upande wetu na kwa upande mwingine lakini wachezaji wamejitahidi wameweza kumaliza nafasi ya pili, tunaamini changamoto ambazo zilizokuwa nje ya uwanja kama zisingekuwepo basi sisi tungechukua ubingwa mapema tu,” alisema Mwakalebela.

Comments are closed.