Yondani Apewa Kazi Maalumu Caf

KOCHA Mkuu wa Klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera, amesema amempa kazi maalumu beki wa timu hiyo Kelvin Yondani ya kuidhibiti safu ya ushambuliaji ya Township Rollers na kuhakikisha haipati mabao.

 

Yanga wameingia jana jijini Dar, wakitokea Zanzibar walikofanya maandalizi ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana utakaopigwa leo Jumamosi kwenye Uwanja Taifa, Dar.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Zahera amesema amempa kazi maalumu Yondani ya kuongoza
safu ya ulinzi na kudhibiti mashambulizi ya Township Rollers.

 

Zahera ameweka wazi kuwa Yondani aliomba mapumziko mafupi baada ya kutoka kwenye majukumu ya timu ya taifa, ndiyo maana hakujiunga na kambi ya Zanzbar.

 

“Nimeongea na Kelvin nimemwambia kuwa yeye ndiye mwenye jukumu la kuongoza safu ya ulinzi akishirikiana na wenzake na kuhakikisha washambuliaji wa timu pinzani hawapati mwanya wa kupita kirahisi,” alisema Zahera


Loading...

Toa comment