The House of Favourite Newspapers

Yusuph Jackson Akabidhiwa Gari lake na SportPesa

YUSUPH Jacksoni Murimi(29), Mkazi wa Serengeti jana alikabidhiwa rasmi gari yake aina ya Renault Kwid mara baada ya kuibuka mshindi kwenye promosheni ya Faidikana Jero.

 

Promosheni ya Faidika na Jero ilidumu kwa siku 40 ambapo watumiaji wa mtandao wa Tigo kupitia huduma ya TigoPesa walipata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo smartphone kila siku na siku ya mwisho zawadi ya gari.

Akizungumza wakati wa makabidhiano, Yusuph alisema kuwa “Ukirudia mazungumzo yangu siku ya kwanza wakati napigiwa simu utagundua kwamba nilikuwa siwaamini walionipigia simu kama ni kweli SportPesa maana siku hizi mjini watu hawatabiriki.

 

“Nilikuwa nacheza tu lakini sikutarajia bahati hii ya ushindi wa gari itanidondokea mimi.

“SportPesa wamenipa mapokezi mazuri ikiwemo kusimamia gharama zote kuanzia usafiri wa ndege, malazi pamoja na matumizi ya siku nzima na kuhakikisha gari langu linapata usajiri kupitia jina langu na kukabidhiwa”

“Sijui nisemeje lakini nawashukuru sana SportPesa, mimi nimuajiriwa kwenye kampuni kama fundi welder nasikutarajia kama siku ningeweza kushinda zawadi ya gari”

“Nawasihi vijana wenzangu wacheze na SportPesa maana kwa sasa nawaona hawana mpinzani, nasio kama unapoteza pesa. Mimi nilikuwa nacheza na kushinda kwa kubashiri mechi kama sehemu ya burudani lakini leo nimejionea dhahiri kuwa kuna zaidi ya ushindi”

 

Kwa upande wa SportPesa, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas alisema “SportPesa inazidi kuwafungulia dunia wateja wake hasa kwa kupitia promosheni mbalimbali kupitia simu ya mkononi unaweza kufanya maajabu yanayoweza kubadili maisha yako.

“Napenda kumpongeza sana, Yusuph kwa ushindi wake nakujinyakulia gari mpya aina ya Renault Kwid na kuweza kuitumia kujiingizia kipato nashughuli nyingine za kujenga taifa.

“Hivyo basi Watanzania wakae mkao wa kula mambo mazuri zaidi yanakuja kutoka SportPesa ili kuwaongezea burudani wateja wetu,”alisema Tarimba.

 

Mwakilishi kutoka Tigo, IkundaNgowi naye alisema “Kwa mara nyingine tena ningependa kumpongeza mshindi wetu na kuwahasa Watanzania waendelee kucheza na SportPesa kupitia mtandao wa tigo maana mambo mazuri ni mengi.

Comments are closed.