The House of Favourite Newspapers

ZAHERA AKATAA MSHAHARAWA SH MILIONI 34

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amewashangaza vilivyo viongozi wa klabu hiyo baada ya kuwaambia kuwa alikataa mshahara wa dola 15,000 kwa mwezi (zaidi Sh 34 milioni) ili tu aendelee kuifundisha timu hiyo na kuhakikisha mipango yake aliyoianzisha inasimama.

 

Zahera ambaye alijunga na Yanga mwishoni mwa msimu uliopita, alisema kuwa timu ya soka ya Buildcon ya nchini Zambia ndiyo Iliyomtangazia dau hilo baada ya kuvutiwa na uwezo wake.

 

Alisema Buildcon ilikuwa tayari kumpatia mshahara huo kwa mwezi lakini kutokana na mapenzi makubwa aliyonayo dhidi ya Yanga pamoja mipango ambayo ameainzisha klabuni hapo, akaamua kuipotezea ofa hiyo.

 

“Jambo hili pia hata kocha Noel Mwandila (kocha msaidizi wa Yanga) analijua kwani baada ya Rais wa Buildcon kunipigia simu na kuniambia juu ya jambo hilo, nilimwambia.

 

“Lakini nilimwambia kuwa sipo tayari kuondoka Yanga kwa sasa na sababu kubwa ni hizo nilizojitaja hapo awali,” alisema Zahera.

Sweetbert Lukonge na Said Ally

 

FULL VIDEO: YANGA Walivyofuturisha Serena Hotel, BAKULI Latembezwa!

Comments are closed.