The House of Favourite Newspapers

Tetesi za Usajili Ulaya

0
Straika wa Arsenal, Olivier Giroud.

STRAIKA wa Arsenal, Olivier Giroud amezungumza na Kocha wa Everton, Ronald Koeman kuhusu uwezekano wa kujiunga kikosini mwake.

REAL Madrid imemwambia straika kinda Kylian Mbappe anayechezea Monaco kuwa watamsajili ikiwa watawauza washambuliaji wake Alvaro Morata na James Rodriguez

Kiungo wa Leicester, Riyad Mahrez.

KIUNGO wa Leicester, Riyad Mahrez anatarajiwa kuanza mazoezi na wenzake kwa ajili ya pre-season lakini Arsenal imepanga kumnasa nyota huyo ambaye anatajwa kuwa na thamani ya pauni milioni 50.

CHELSEA inadaiwa ipo kwenye mchakato wa kumnasa straika wa Swansea, Fernando Llorente. Antonie Conte na Llorente wanaripotiwa kuwa kwenye uhusiano mzuri tangu walipokuwa pamoja Juventus hivyo kuna uwezekano wakaungana tena pale Darajani.

KIDUCHU! Ndivyo unaweza kusema baada ya Barcelona kutolewa ‘mkuku’ na pauni milioni 22 ilizotaka kuwapa Wachina wa Klabu ya Guangzhou Evergrande wakitaka wapewe kiungo, Paulinho, 28.

Romelu Lukaku.

ROMELU Lukaku amekubali mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki pale United huku dau lake likitajwa kuwa pauni mil 75 lakini Chelsea imejipanga kuiendea mbele zaidi Man U ili kuhakikisha inamrudisha ‘nyumbani’ straika huyo anayemilikiwa na Everton.

IMRIPOTIWA Arsenal wala haijapeleka ofa yoyote kwa kiungo wa Napoli, Jorginho, hii ni kwa mujibu wa wakala wake.

LIVERPOOL imepewa makavu baada ya kuambiwa kuwa kiungo wanayemfuatilia kwa ukaribu, Naby Keita wa Leipzig wala hatouzwa kwa kuwa klabu hiyo haina mpango wa kuuza wachezaji tegemeo wa kikosini humo.

Leave A Reply