
BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Idd Pialali ni mmoja kati mabondia watatu wa Tanzania watakaopanda ulingoni Julai 22, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem katika mapambano ya Ubingwa wa Global Tv, Afrika Mashariki na Kati yatakayorushwa mushabara na kituo hicho.
Idd Pialali: Njooni Dar Live Mshuhudie Nitakavyomuua Mkongo
Katika mapambano hayo ya kimataifa, yaliyoandaliwa na kampuni ya kupromoti mchezo wa ngumi za kulipwa nchini, Solid Rock Tanzania ambayo yatasimamiwa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO) chini ya rais wake, Yassin Abdallah ‘Ustaadh.
Pialali anayetumia mguu wa kushoto ‘orthodox’ katika masumbwi hayo yatakayorushwa mubashara na Kituo cha Global TV Online kupitia website yake ya www.globaltvtz.com atacheza na bondia Regin Champion wa DR Congo, Nasibu Ramadhan ‘Pacman’ akicheza na Mzimbabwe, Tinashe Mwadziwana huku Miyeyusho akitarajia kumalizana na Israel Kamwamba wa Malawi.

Katika mahojiano maalum na Risasi Jumamaosi, Pialali ameweza kufunguka mipango yake na sababu iliyomfanya awe bondia wa ngumi za kulipwa:
“Baba ndiye alinifanya niingie katika michezo maana yeye alikuwa anacheza karate, akanichukua katika mchezo huo lakini binafsi sikuwa nimeupenda, mjomba wangu anayeitwa Pialali alikuwa anacheza ngumi ndiye aliniambia niingie huko.
“Kiukweli kwenye ngumi nilianza vizuri chini ya kocha wangu, Edward Emmanuel ambapo nilianzia katika ngumi za ridhaa huko nikapiga mabondia wengi.
“Nikaenda Uganda lakini nikapigwa nusu fainali ila niliwakilisha vizuri baada ya hapo nikawa navizia ajira jeshini, sikuweza kupata ajira nikaamua kuingia katika ngumi za kulipwa ambapo nimeweza kucheza mapambano 22.
“Mpaka sasa nina mkanda wa Ubingwa wa WBC,IBF, WBO na mkanda wa Tanzania, Jumla nina mikanda minne ambayo nimefanikiwa kuchukua tena.

UMEJIPANGA VIPI KUELEKEA KATIKA PAMBANO LA MKONGO?
“Nimejipanga vizuri sana, sijamuona mpinzani wangu ila bado naendelea kumfuatilia kupitia katika vyanzo vyangu kwa kuweza kupata taarifa zake lakini nitahakikisha hatoki salama kwenye ardhi yetu ya Tanzania yaani nitampiga tu!
“Najiamini kwa sababu nina uwezo wa kutosha, nimepigana muda mrefu kwenye ngumi za ridhaa, natumia akili nyingi ulingoni hata akiwa na mwili kama nyumba lazima atakaa tu hilo halina ubishi.
“Mwalimu wake ajiande vizuri kwa kubeba jeneza kwa sababu lengo langu ni kumuua ndani ya ulingo.
“Nashukuru viongozi na makocha wangu wananiongoza vizuri ndiyo maana nina uhakika kuwa hatachomoka katika mikono yangu tena kwetu mbele ya Watanzania, sitawaangusha.
NI KWELI WEWE NDIYO MRITHI WA THOMAS MASHALI ‘SIMBA ASIYEFUGIKA’?
“Siwezi kujua kama nimemrithi Simba ila wanaosema ni mashabiki ambao wao ndiyo wananielewa vyema kwa sababu marehemu alikuwa anatumia sana akili ya kuweza kuwapiga watu kutokana na ‘foot work’ aliyokuwa nayo kitu ambacho hata mimi ninacho.
“Kitu kingine ambacho wanasema ninacho kutoka kwa Mashali, alikuwa anatumia akili nyingi kuliko bondia yeyote wa Tanzania, nadhani ndiyo sababu ya kusema hivyo ikiwemo na uwezo wangu wa kushambulia huku nikiwa natembea.

KUNA TOFAUTI GANI KATIKA NGUMI ZA KULIPWA NA RIDHAA?
“Utofauti ni mkubwa kwa sababu huwezi kuibuka kuwa bondia bora kama hujapita katika ngumi za ridhaa maana ndiyo kuna msingi wa ngumi zenyewe licha ya hivyo ndiyo zinatoa uzoefu wa faida, mimi sina muda mrefu kwenye ngumi za kulipwa lakini angalia rekodi ambayo nimeshaitengeneza hadi sasa.
“Kuna bondia kama Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ anafanya vizuri katika mapambano yake kwa sababu ameanzia katika ngumi za ridhaa ila kama utaanzia moja kwa moja katika ngumi za kulipwa huwezi kuwa bondia bora.
Video: Nasib Ramadhani Nitampiga vibaya Mzimbabwe Njooni Dar Live

UNAWAAMBIA NINI MASHABIKI WAKO KUELEKEA KATIKA PAMBANO HILO?
“Binafsi nimezoea katika mapambano ya ndani kwenda na mashabiki wangu kwa ajili ya kunipa sapoti ila nina uwezo wa kucheza pambano katika mazingira yoyote na nikacheza vizuri, nimeshaenda nje mara kibao na nikacheza vyema bila ya uwepo wao.
“Kikubwa wao ambacho wanatakiwa kufanya hivi sasa ni kuhakiksha wanaingia katika website ya www.globaltvtz.com ili kuweza kuona live kupitia Global TV Online.
“Wanachotakiwa kufanya ili kuweza kuona live kwenye simu zao ni kuingia katika hiyo website au katika Mtandao wa YouTube kisha waandike Global TV Online na wata-subscribe, baada ya hapo pembeni wataona alama ya kengele ambayo wataibonyeza na moja kwa moja wataweza kupata matukio yote ya Global TV papo hapo na kuliona pambano langu siku hiyo kutokea Dar Live wakiwa majumbani mwao,” anasema Pialali.

Katika hatua nyingine, pambano hilo la ngumi za kimataifa halitakuwa na kiingilio na mashabiki wataweza kulishuhudia mubashara (LIVE) kupitia simu zao za mkononi tu, kwani litaonyeshwa na Global TV pekee. Wadau na mashabiki watakaopata nafasi ya kuingia ukumbini wataingia kwa kadi maalum za mwaliko tu.
Kwa kuwapa hamasa mabondia wa Tanzania watakaopambana siku hiyo, jana Ijumaa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO) chini ya rais wake, Yasin Abdallah ‘Ustaadh’ iliianika mikanda itakayowaniwa.

Ili kulishuhudia pambano hilo kwa njia ya simu tena bure, hakikisha unajiunga (subscribe) na YouTube Chanel ya Global TV Online sasa hivi ili usipitwe. Ingia You Tube, tafuta GLOBAL TV ONLINE, kisha bonyeza neno subscribe pia bonyeza kikengele kidogo kilichopo pembeni yake ambacho kitakukumbusha kuangalia pambano hilo mara tu litakapoanza.
Kama wewe umeshajiunga, basi hakikisha pia umebonyeza kikengele ili usipitwe na kila kinachoendelea Global TV. Pia unaweza kutupata kupitia mtandao wetu wa www. globaltvtz.com. Usisubiri, jiunge sasa na Global TV ili uwe wa kwanza kuona ndondi za kimataifa. KAJIUNGE SASA kwa kubonyeza HAPA: www.youtube. com/user/uwazi.
MAKALA: IBRAHIM MUSSA, DAR