The House of Favourite Newspapers

Kocha Simba: Okwi, Bocco Watavunja Rekodi Yanga

1
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi .

KOCHA Msaidizi wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja, ameweka wazi kuwa ana imani kubwa kuwa washambuliaji wao, Emmanuel Okwi na John Bocco wataivunja rekodi ya kufunga mabao mengi ambayo kwa misimu miwili mfululizo imekuwa ikishikwa na wapinzani wao, Yanga.

Simba walifunikwa na Yanga katika msimu uliopita katika kipengele cha ufungaji bora ambapo Yanga walifunga jumla ya mabao 57 yakiwa saba mbele ya wapinzani wao Simba waliofunga mabao 50.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Mayanja amesema kuwa endapo washambuliaji hao wakiwa fiti kwa asilimia 100 basi wanaweza kufunga mabao mengi kuliko ya wapinzani wao Yanga.

“Kama kombinesheni ya Bocco na Okwi ikienda vyema, basi nina uhakika kabisa wa Simba kufunga mabao mengi tofauti na msimu uliopita ambapo Yanga walitupita kwenye suala la kufunga mabao mengi.

“Naamini kama wachezaji hao wakiwa fiti mwanzo mwisho wa ligi, basi watatisha sana kwani kila mmoja anafahamu uwezo wao kwenye suala zima la kuwafunga wapinzani,” alisema Mayanja.

Stori: Sweetbert Lukonge | Championi Jumatano

1 Comment
  1. […] ikiwa na Bocco na Okwi na Mghana  Nicolas Agyei Simba haiwezi kupoteza, si sahihi hata […]

Leave A Reply