The House of Favourite Newspapers

MSIJIDANGANYE, SIMBA HAIJASAJILI MALAIKA

0

 

Wachezaji wa Simba wakifanya mazoezi.

MASHABIKI wa Simba, leo watamiminika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Tamasha la Simba Day wakiwa na shauku kubwa. Shauku kubwa ya mashabiki hao ni kutaka kuona timu yao “mpya”. Wengi wangependa kutumia neno mpya kwa kuwa wachezaji wapya wamesajiliwa na wangependa kuwaona kwa mara ya kwanza wakiwa uwanjani na kikosi hicho.

 

Binadamu yeyote, kisaikolojia hupenda kushuhudia jambo linalomfurahisha kwa macho yake. Yaani angependa macho yaone badala ya masikio kusikia wakati akihadithiwa. Huenda baadaye angependa k u o n a mdomo wake unafanya kazi ya kuhadithia ukichukua yale ya kutoka katika picha ya macho yake, akiwagawia wengine.

 

Watakaokwenda kuiona Simba kwa mara ya kwanza, hasa kwa mashabiki wa klabu hiyo, kitu kikubwa ambacho kitawafurahisha zaidi ni kama kikosi chao kitaondoka na ushindi katika mechi ya kirafi ki dhidi ya mabingwa wa Rwanda, Rayon Sports. R a y o n Sports, si timu ya kubeza ingawa suala hilo linaweza kuwa si jambo kuubwa sana. Matumaini ambayo mashabiki wa Simba wamebeba kutokana na kikosi chao cha Simba ni kupata ushindi.

Niyonzima (kushoto) akifanya mazoezi kwa kufuata maelekezo ya kocha msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja.

Huenda wako ambao wanaamini ambayo si sahihi na huenda hawajui kama wanayoamini si sahihi katika mpira na kama wakiendelea kuyatanguliza kama imani inayowaongoza, baadaye wanaweza kuumia, wakianzia kuchukua maumivu katika mioyo yao na baadaye ubongo.

 

Wako wanaoamini usajili wa msimu huu wa Simba ni wa kufa mtu na timu yao ni lazima ichukue ubingwa, hilo ni kosa kubwa sana. Ligi si kitu cha lelemama na kama wanapima hivyo, wana uhakika gani Simba haitafungwa au kuharibu?

Mayanja akimnyoosha viungo, Niyonzima.

KOSA NAMBA 1:

Uhakika wa kuwa Simba ni bingwa utapimwa na nguvu ya vikosi vingine baada ya ligi kuanza.

Watakaokwenda kuiona Simba kwa mara ya kwanza, hasa kwa mashabiki wa klabu hiyo, kitu kikubwa ambacho kitawafurahisha zaidi ni kama kikosi chao kitaondoka na ushindi katika mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Rwanda, Rayon Sports. R a y o n Sports, si timu ya kubeza ingawa suala hilo linaweza kuwa si msimu huu wa Simba ni wa Mashabiki wanaweza kuendelea kuisapoti timu yao halafu mwisho wanaamini inatakiwa kupambana hasa ili kuwa bingwa na ubingwa hautakuwa kama mtu anayechuma pera kutoka kwenye mti wake uliozaa katika eneo lisilo na urefu mkubwa.

 

KOSA NAMBA 2:

Kusajiliwa kwa Emmanuel Okwi kunawafanya mashabiki wengi kuamini sasa Simba haitakamatika na hakuna anayeweza kuizuia. Kuamini hivyo ni kosa la pili, ndiyo maana nimeamua kutumia msemo wa hivi; Simba haijasajili malaika. Okwi n i mwanadamu, anawezekana kuzuiwa na kuna siku hatakuwa katika kiwango kizuri akashindwa kucheza vizuri au kuwa msaada katika kikosi.

 

Okwi alikuwa Simba, haikuwa bingwa. Anaweza kuwa msaada mkubwa akipata ushirikiano mkubwa na muongozo sahihi lakini hawezi kuwa ‘garantii’ ya Simba kushinda kila siku.

 

KONA NAMBA 3:

Uhakika wa kuwa na washambulizi wakali kama John Bocco, unasikia mashabiki wengi wanasema “watu watapigwa tanotano”, hili ni kosa jingine. Nasema hivyo kwa kuwa Simba siku moja itapoteza ikiwa na Bocco na wote kwa kuwa soka ndivyo ilivyo, utashangaa nini kwa Simba wakati hata Real Madrid inapoteza Cristiano Ronaldo akiwa uwanjani au Barcelona inalala Lionel Messi uwanjani!

 

Kuamini ikiwa na Bocco na Okwi na Mghana  Nicolas Agyei Simba haiwezi kupoteza, si sahihi hata kidogo.

 

KOSA NAMBA 4:

Simba imesajili makipa wapya hasa Aishi Manula kutoka Azam FC na Said Mohamed ‘Nduda’ aliyekuwa Mtibwa Sugar. Hii inawafanya mashabiki wengi wa Simba, waamini Simba haiwezi kufungwa hata mechi moja.

 

Angalia Manula aliruhusu mabao mangapi msimu uliopita, halikadhalika Nduda akiwa na Mtibwa Sugar. Sasa akiwa Simba kwa nini asifungike. Hata kama itafanya vizuri sana, lakini Simba itafungwa tu na huu ndiyo mpira ulivyo.

 

KOSA NAMBA 5:

Baada ya usajili wa Niyonzima kukamilika, shabiki wa kawaida anaweza kuwaza Mnyarwanda huyo akiwa na Jonas Mkude, pia James Kotei, Simba itapotezaje?

 

Hili kosa pia. Simba inaweza kuwa imara kutokana na kuwa na watu bora, lakini hili halitoi uhakika wa asilimia 100 kutofungwa na makosa hufanywa na wanadamu. Hawa walio bora ni wanadamu, wanaweza kukosea wakati wowote.

 

Kuendelea Simba haiwezi kupoteza ni kutengeneza maumivu ya baadaye na kwa mashabiki wanachotakiwa kufanya ni kazi yao na iwe chanya. Kuwa chanya, nazungumzia ile hali ya mashabiki wengi kujisahau na kuingia katika kazi za wachezaji au makocha wakiamini wanajua zaidi yao.

 

Huenda kufanya kazi yao ya kuiunga timu yao mkono kwa nguvu inaweza kuwa msaada mkubwa zaidi tena wakaonyesha moyo wa kuendelea kuunga mkono kwa nguvu hata pale wachezaji wao wanapokuwa wameteleza, mfano wametanguliwa kufungwa au wamepoteza, halafu wakaendeleza kuunga mkono, hii itazidi kuwafanya wachezaji wajitume zaidi wakiamini kuna watu wanaowaangusha na haitakuwa sahihi kuwaangusha tena.

 

Kuamini sana ni vizuri kwa kitu chochote lakini katika soka, lazima kuamini na kuweka nafasi ya kupata kile ambacho hukukitegemea na nini cha kufanya kilicho bora kama hali hiyo haijatokea.

Na: Saleh Ally| Champion Jumanne

Leave A Reply