Giggy Amuwakia Mzee Majuto
VIDEO queen ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amemuwakia lejendari wa vichekesho Bongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ kwa kumchana tabia yake (Gigy) ya kupiga picha za utupu na kuposti mitandaoni.
Gigy aliiambia 3-Tamu kuwa, anamshangaa Mzee Majuto kwa kumfuatilia maisha yake na kama hapendi, basi asiangalie picha zake.
“Kama hapendi swaga zangu ya nini asumbuke kutazama picha zangu. Hayo ndiyo maisha ngu niliyochagua, akiyafuatilia, ataumia kichwa bure, sioni cha ajabu kwangu kwa sababu kuna wasanii wengi tu wanakaa utupu,” alisema Gigy ikiwa ni siku chache tangu Mzee Majuto alipomtaka kuacha tabia hiyo.