Walipomaliza kufanya yao, kila mmoja alikuwa hoi, walibaki wakiangaliana kama majogoo yaliyotaka kupigana. Ingawa katika maisha yake alitembea na wanawake wengi, ila siku hiyo sasa, alikuwa hoi, jalamba alilopelekwa likamfanya kuwa taabani.
“Kweli nimeamini vuka mto utukane mamba, manaake ulivyonipelekesha, kweli mzee mwenzangu anafaidi,” alisema baba Fanueli huku akimwangalia mama Zubeda usoni.
“Umeridhika sasa?” aliuliza mama Zubeda.
“Kuridhika nimeridhika, ila kama kutatokea nafasi ya pili, kwa nini nisitake?”
“Kwa hiyo unataka tena?”
“Kwani dhambi? Wewe nipe tu na mimi nijimwae,” alisema baba Fanueli.
Hapohapo mama Zubeda akamsogelea baba Fanueli na kumlaza chali, alitaka kumfanyia makeke mengi, kumpagawisha mzee wa watu mpaka akiri kwamba hakuwahi kukutana na mwanamke mwenye uwezo mkubwa kama wake.
“Nataka nikupe yenyeweyenyewe sasa,” alisema mama Zubeda.
“Unasemaje?”
“Kwani umesikiaje?”
“Kwa hiyo ile ya kwanza….
“Hiyo ilikuwa trela, sasa muvi ndiyo linaanza, tena muvi la Kihindi, saa tatu mpaka nne,” alisema mama Zubeda, baba Fanueli akashtuka.
“Nitapona kweli?”
“Kwani hauna pumzi?”
“Pumzi ninazo.”
“Sasa unaogopa nini?”
Raundi hii ya pili ndiyo ilikuwa kiboko, kama ni mechi uwanjani basi timu moja inashambuliwa dakika zote tisini huku ikichezewa nusu uwanja. Baba Fanueli alichoka lakini hakutaka kuonesha udhaifu, kila mashambulizi yalipopelekwa kwake kwa kasi, aliyarudisha hivyohivyo, alishindwa, pumzi ilikata ila alitaka kwa dakika tisini hata suluhu atoe.
“Hapa vipi baby? Hapa je? Hapo kupoje? Na huku napo baby?” aliuliza mama Zubeda, wakati huo alikuwa juu ya baba Fanueli, alizunguka kama pangaboi ya Mjerumani, mikono yake ilikuwa katika mbavu za baba Fanueli, mtu mzima akawa hoi.
“Subir…” alisema baba Fanueli huku akili kama mtoto.
“Nisubiri nini jamani baby….”
“Unataka kuondoka nayo?” aliuliza baba Fanueli huku akihema juujuu kama mbwa aliyekosa chakula.
“Kwani nikiondoka nayo kuna tatizo?”
“Hakuna ila…..utaniua na uzee huu.”
“Ila si umetaka mwenyewe! Subiri mpaka ukate kiu yangu! Mwenzako ndiyo kwanza nimeanza,” alisema mama Zubeda. Akajikoki, kilichofuata, ni kelele za raha na karaha, kitanda kililalamika kana kwamba chaga zilitaka kuvunjika, mama Zubeda hakuacha, muda wote huo alimpeleka puta mzee wa watu.
****
“Una habari shoga?”
“Wala sina! Kuna nini?”
“Hahaha! Haloo…”
“Mbona unacheka sasa? Kuna nini?”
“Yaani upo umekaa bila kuwa na habari shoga’angu, pole yako.”
“Hebu subiri kwanza, mbona unanitia presha, kuna nini?”
“Manzese hiyooo…”
“Manzese…kumefanyaje?”
“Hujui kama kikulacho ki’nguoni mwako?”
“Unamaanisha nini shoga’angu?”
“Watu wapo Manzese sasa hivi, wanakonga nyoyo zao, wewe upo tu huku kama mdoli….watu wanajilia vyao tu huko.”
“Unanichanganya! Hebu niambie kwanza, kuna nini mbona unataka kuniua kwa presha…”
“Mumeo yupo wapi?”
“Alitoka!”
“Kwenda wapi?”
“Sijui ila alitoka!”
“Hahaha! Unalo hilo.”
“Mama Halima, hebu niambie kuna nini!”
Ukiachana na mama Zubeda, mwanamke mwingine aliyekuwa akiongoza kwa umbeya mtaani hapo alikuwa mama Halima. Kila wakati masikio yake yalisimama kama popo, alitega habari, aliposikia hili, harakaharaka alilipeleka kwa watu wengine.
Siku hiyo alikuwa zake Manzese, akiwa hana hili wala lile, ghafla akamuona baba Fanueli akishuka kutoka kwenye Bajaj na kuingia ndani ya gesti bubu moja. Alimjua mzee huyo kwa tabia yake ya kunusanusa kwa kila mwanamke, akajua kuna jambo, hivyo akasubiri kuona nani angefuata.
Baada ya saa moja, mama Zubeda huyo mjengoni, alishtuka kwani alijua kwamba mama Zubeda na mama Fanueli walikuwa marafiki, ilikuwaje leo hii mwanamke huyo alitaka kuvunja ushosti kwa kutembea na mume wake, ndiyo akaupeleka umbeya uliomfanya mama Fanueli kuhema juujuu.
“Niambie kwanza, kuna nini?” aliuliza mama Fanueli, tayari akaanza kupandisha mori kama Mmasai.
“Sisi wanawake ni watu wabaya sana.”
“Kwa nini? Mbona unaniweka roho juu mwenzio?”
“Hivi una uhakika kwamba mumeo hajakuaga?”
“Ndiyo! Hebu niambie kuna nini?’
“Mumeo nimemuona Manzese.”
“Manzese! Anafanya nini?”
“Aliingia kwenye gesti moja hivi, ipo ndanindani kabisa.”
“Kaingia gesti?”
“Ndiyo! Tena baada ya muda na rafiki yako akaingia,” alisema mama Halima.
“Unanichanganya shoga’angu!”
“Ndiyo hivyo! Yaani ninavyokwambia sasa hivi, tuandae madela mama Zubeda akija tukamsute…”
“Unasemaje?”
“Mama Zubeda anatembea na mumeo. Hapa ninavyoongea, wapo ndani wanafanya yao,” alisema mama Halima huku akijiona bingwa wa kutoa habari.
“Haiwezekani! Mama Zubeda hawezi kunitenda hivyo…”
“Halooo halooo…eti hawezi! Unalo hilo,” alisema mama Halima.
“Hebu niambie gesti hiyo ipo wapi.”
“Unataka kwenda?”
“Ndiyo!”
“Ngoja nikajiandae, nikawaandae na mashosti wengine twende, tena tuvae na madela yetu ya sare.”