×

Idris Ageuka Bodigadi Wa Mnamibia!

idris na mnamibia (1)
MSHINDI
wa Shindano la Big Brother Africa ‘Hotshots’ 2014, Idris Sultan juzi kati aligeuka bodigadi wa muda wa mshiriki mwenzake wa Big Brother kutoka Namibia, Luis Munana.

idris na mnamibia (2)Katukio hako ‘amazing’ kalijiri katika sherehe ya kuzaliwa ya staa wa Bongo Movie, Wema Sepetu ambapo muda mwingi Idris alikuwa akihakikisha Mnamibia huyo anakuwa katika ulinzi wa kutosha na hakuna mtu anayeleta purukushani kwake.

idris na mnamibia (4)“Ilikuwa kama vituko, kuna muda Mnamibia aliitwa na Wema kwenda kulishwa keki, kuonesha kwamba ni bodigadi wake, Idris akamtuliza na kumwekea kitambaa maalum kifuani asije kujichafua,” alisema mmoja wa wahudhuriaji.

Leave a Comment