Mastaa Wamwandama Dk. Fadhili
KUFUATIA elimu yake ya kisasa ya jinsi mwanamke yeyote mwenye uzazi anavyoweza kupata watoto mapacha, Dk. Fadhili Emily wa Kitengo cha Sayansi na Tiba Asilia Clinic kilichopo Mbezi Afrikana, ameanza kuandamwa na baadhi ya mastaa wakitaka kukutana naye ‘laivu’ kwa ajili ya kuwapa somo hilo kwa ufasaha zaidi.
Akuzungumza na Ijumaa Wikienda juzi, Dk. Fadhili alisema mastaa kibao (hakuwataja majina) wamekuwa wakimpigia simu na kumpa mwaliko majumbani mwao ili akawafundishe kwa ufasaha somo la jinsi ya kupata watoto mapacha.
“Lakini hata hivyo wakae tayari. Naandaa siku moja maalum ambapo mastaa wote nitawaalika mahali maalum na kuwafundisha kwa pamoja badala ya kwenda kwa mmoja mmoja,” alisema daktari huyo.
Hata hivyo, zipo taarifa za chinichini kuwa, baadhi ya mastaa waliowahi kumpigia simu Dk. Fadhili kwa lengo la kupata elimu ya kuzaa mapacha ni Rose Ndauka, Jacqueline Wolper (anayedaiwa ‘kutoka’ naye), Aunt Ezekiel, Mayasa Mrisho ‘Maya’ na Kulwa Kikumba ‘Dude’ ingawa wote walipotafutwa na gazeti hili walikanusha lakini wakikiri kutaka kuijua elimu hiyo kwa undani.


