Bodaboda yamvunja bega Masai Nyota Mbofu
Msanii wa Vichekesho, Gilliady Severine ‘Masai Nyota Mbofu’.
MSANII wa Vichekesho aliyewahi kutamba na Kundi la Vituko Show, Gilliady Severine ‘Masai Nyota Mbofu’, amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuvunjika bega kufuatia ajali mbaya ya pikipiki (Bodaboda) kugongana na gari la kuinulia vitu vizito (forklift).
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni maeneo ya Magomeni jijini Dar ambapo msanii huyo alikuwa akiendesha bodaboda akitokea maeneo ya Gongo la Mboto na baada ya kufika Magomeni-Usalama alishangaa ghafla kuchomekewa na forklift na kusababishia ajali hiyo.
Akizungumza na Amani, Masai alisema kuwa baada ya ajali hiyo alikimbizwa katika Hospitali ya St. Monica, Manzese-Darajani jijini Dar na kupatiwa matibabu.
“Namshukuru Mungu ilikuwa nisiwepo duniani. Kwa sasa naweza hata kuongea japokuwa nilipoletwa hapa hali yangu haikuwa nzuri hata kidogo,” alisema Masai.

