Staa mwenzake wa muziki wa Pop, Selena Gomez akiwa na mpenzi wake Niall Horan.
STAA wa kundi la One Direction, Niall Horan ameweka wazi uhusiano wake wa kimapenzi na staa mwenzake wa muziki wa Pop, Selena Gomez.
Kwa mujibu wa chanzo, Niall ameweka wazi uhusiano wake kwa kutubu kuwa hatokuja kumfanyia mchezo ama kumliza Selena katika mapenzi kama alivyowahi kufanya mpenzi wake wa zamani, Justin Bieber.
“Selena alikuwa hataki kabisa kujiingiza katika uhusiano wa kimapenzi kwa kipindi hiki, alihofia yatakuja kujitokeza kama yale ya Bieber (Justin), lakini Niall ametubu yote, amemuahidi atamfanya kuwa na furaha muda wote wa mapenzi yao,” kilisema chanzo.
(Imeandaliwa na Andrew Carlos/gpl)