MSANII wa muziki wa Soul kutoka Nigeria, Aituaje Iruobe ‘Waje’ ambaye anatamba na Wimbo wa Onye aliomshirikisha Tiwa Savage, amefunguka kuwa kati ya sehemu ambazo anatamani sana kuzibadilisha mwilini mwake ni matiti yake kutokana na ukubwa yaliyonayo.
Waje amefunguka hayo hivi karibuni kupitia Kipindi cha MTV Base kiitwacho Real Talk na kuongeza kuwa mbali na matiti yake kitu pekee anachojivunia ni uzuri wa ngozi aliyonayo ambayo ana mahaba nayo kupitiliza kiasi kwamba hutumia gharama nyingi kuitunza.
“Nafurahia sana weusi wa mng’ao wa ngozi niliyonayo lakini kitu pekee ambacho huwa sivutiwi nacho na ningependa kubadilisha hata sasa ni matiti yangu,” alisema Waje.