×

Mzazi mwenza achokonoa ndoa ya Jack Chuz

JACK3Msanii wa filamu za Kibongo, Jacqueline Pentzel akiwa na mumewe Gardner Dibibi.

Na Gladness Mallya
KERO! Baada ya kurudiana na mumewe Gardner Dibibi, msanii wa filamu za Kibongo, Jacqueline Pentzel maarufu kama Jack Chuz, mzazi mwenza wa mume wake anadaiwa kuichokonoa ndoa yao hivyo kumpa kero.

Chanzo makini kililiambia gazeti hili kwamba, Jack Chuz na mumewe wamekuwa wakitibuana chanzo kikiwa ni mwanamke aliyezaa na mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina moja la Mariamu, kwani amekuwa akiwafuatilia kila wanachokifanya huku akiendelea kumsumbua Dibibi akitaka warudiane.

Paparazi wetu alimtafuta Jack Chuz ili kupata ukweli na yeye akafunguka hivi;
“Kiukweli Mariamu anamsumbua sana mume wangu, naomba atuache tule starehe zetu kwani anampa matumizi ya mtoto kama kawaida, lakini amekuwa akitufuatafuata hata tukitoka out kesho yake anampigia simu na kumuuliza, huku mara nyingi akimuomba warudiane.”

Leave a Comment