×

Wasanii wakongwe wa filamu wamtaka Mwakifwamba  aendelee  kuwa rais wao

1.Kutoka kushoto ni wasanii wakongwe wa kuigiza, Ramadhan Mrisho, Ahmed Olotu (Mzee Chilo) na Salome Sokoni (Mama Abdul.

Kutoka kushoto ni wasanii wakongwe wa kuigiza, Ramadhan Mrisho ‘Mashaka’, Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’ na Salome Sokoni ‘Mama Abdul’.

2.Msanii mkongwe wa maigizo, Salome Sokoni Nonge 'Mama Abdul' aliyoko kulia akitoa ufafanuzi wa jambo.

Msanii mkongwe wa maigizo, Salome Sokoni Nonge ‘Mama Abdul’ aliyeko kulia akitoa ufafanuzi wa jambo.

3.Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.

Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.

4.Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

WAKONGWE wa Filamu hapa nchini, wakiongozwa na Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’ wamemtaka Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba kugombea tena nafasi yake ya urais kwa mwaka 2015  ili awe kiongozi wao tena.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) mmoja wa wakongwe wa filamu, Ahmed Olotu ‘ Mzee Chilo’ akiwa ameambatana na wasanii wenzake ametoa tamko kuwa wanamtaka Mwakifwamba agombee tena urais wa shirikisho hilo.

Mzee Chilo amesema kuwa kauli ya Mwakifwamba ya kusema kuwa hatagombea tena nafasi hiyo wao kama wasanii wakongwe wanapingana nayo kwa kusisitiza  abadilishe fikra hizo kwani wameona nuru imekaribia kwao ya kuendelea kupata mafanikio kupitia kwake.

‘’Tunapinga uamuzi wake na kumuomba abadilishe fikra hizo na agombee tena kwani tumeona nuru imekaribia kwetu baada ya muda mrefu kukosa kitu kinachotuweka pamoja,’’ amesema Mzee Chilo.

Alifafanua kuwa wameshuhudia miradi mingi imeasisiwa chini yake na haijakamilika vyema hivyo aingie tena kuimalizia kazi aliyoianza huku akitoa mfano wa mradi wa ‘TAFF TRUST FUND na TAFF CREATIVE LTD’ ambayo inahitaji umakini mkubwa katika kuhakikisha inasimama na kuwasaidia  wasanii na sera ya filamu inayosubiri kupitishwa na serikali.

Alieleza kuwa TAFF TRUST FUND ni mfuko wa wasanii wa filamu ambao utasaidia katika utendaji wa shughuli zao za kifilamu.

(NA DENIS MTIMA/GPL)

1 Comment

Leave a Comment