
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo, jana (Jumanne) aliwaahidi wakazi wa Nakasangwe Kata ya Wazo Hill, Dar es Salaam, kumaliza mgogoro wa ardhi uliokuwa ukiwakabili kwa kuwapatia hati halali za kumiliki ardhi hiyo.

Hatua hiyo itamaliza mgogoro huo uliochukua muda mrefu, jambo ambalo liliwafanya wakazi hao kushangilia uamuzi huo.

Matatizo mengine aliyoahidi mkuu huyo wa wilaya kuyamaliza ni pamoja na tatizo la maji ambapo alifika eneo hilo na maofisa wa mamlaka ya maji jijini Dar es Salaam (Dawasa) na shirika la umeme nchini (Tanesco) ambao walieleza mipango ya kusambaza huduma hizo kwa wakazi hao ndani ya siku chache.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL